Kamati ya mashindano ya chama cha soka cha Hispania, imempunguzia adhabu ya kadi nyekundu sentahafu wa Real Madrid, Sergio Ramos ambapo sasa atakosa mechi moja tu badala ya  tatu.

Nahodha huyo wa Real Madrid alilambwa kadi nyekundu Jumapili usiku baada ya kumchezea rafu ya miguu miwili Lionel Messi wa Barcelona.

Baada ya mchezo huo wa Clasico, Ramos alisema: "Kadi nyekundu haikuwa halali. Sikukusudia kumuumiza mtu na sikumgusa. Ilistahili kuwa kadi ya njano".

Sasa Ramos atakosa mchezo wa La Liga  Jumatano dhidi ya Deportivo. 


USISAHAU KUBONYEZA SUBSCRIBE HAPO
LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK Saluti5

Post a Comment

 
Top
Nicolaus Trac