KHADIJA YUSSUF AAHIDI ‘KUWAFUNGIA MBWA BANDANI’ JUMAPILI HII TRAVERTINE


Mwimbaji nyota wa taarab Khadija Yussuf “Chiriku” ameahidi kuwafungia mbwa bandani katika mpambano wa Nani Zaidi utakaofanyika Jumapili hii ndani ya Travertine Hotel Magomeni jijini Dar es Salaam.

Jumapili hii ya April 30 kutakuwa na mchuano mkali wa waimbaji nyota watano wa muziki wa taarab Fatma Mchauruko wa Yah TMK, Khadija Yussuf wa Wakali Wao, Hanifa Maulid “Jike la Chui” akiwa na Funga Kazi, Mwamvita Shaibu kutoka Ogopa Kopa na Mwasiti Kitoronto wa Jahazi ambao wataumana kutafuta nani mkali zaidi ya mwenzie.

Kama ilivyoelezwa hapo awali waimbaji hao watapigiwa ‘live’ na bendi zao - Yah TMK, Wakali Wao, Funga Kazi, Ogopa Kopa na Jahazi Modern Taarab.

Khadija Yussuf ametamba kuwa waimbaji wote hao hawajui historia yake wala hawajui lini ameanza kuimba na hivyo atawafundisha kazi na atawafanya kama vile anavyofungia mbwa bandani.

“Mje muone namna navyofungia mbwa na mwenye mbwa bandani, hawa wote hawajui nimeanza lini kuimba. Nitawafundisha kazi siku hiyo,” anatamba Khadija Yussuf.


Onyesho hilo litasindikizwa na Khadija Kopa na Kivurunde huku ma MC wakiwa ni Dida na Dr Kumbuka.

No comments