KIHISPANIA CHAMTATIZA KIUNGO MTANZANIA FARIDI MUSSA

KIUNGO wa timu ya Tenelife ya nchini Hispania, Mtanzania Farid Mussa amesema kwamba lugha ya Kihispania imekuwa tatizo kwake hali iliyomlazimu kutumia mtandao wa simu yake ili kutafsiri wakati anapozungumza na wenzie.

Farid ambaye kabla ya kutimka Ulaya alikuwa akichezea timu ya Azam, anakuwa Mtanzania wa tatu kucheza soka Ulaya baada ya Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu ambaye yupo nchini Sweden.

“Timu yangu ndiyo msaada kwangu, nikiwa na shida naandika kwa lugha ya Kingereza kisha natafsiri Kiispania ndipo namuonyesha mwenyeji kwa ajili ya kunisaidia,” alisema winga huyo.

Lakini hata hivyo tupo kwenye mipango ya kusoma lugha ya Kihispania ili kulaisisha mawasiliano maana imekuwa tatizo, nalazimika kutembea na simu wakati wote,” aliongeza Faridi.


Safari ya Faridi kuelekea nchini Hispania ilifunikwa na hali ya sintofahamu baada ya mchakato mzima kuchukua muda mrefu hali iliyoanza kuwakatisha tamaa Watanzania.

No comments