KIMYA CHA MATAJIRI KATIKA KUINUSURU YANGA SC CHAWASIKITISHA WANACHAMA

KLABU ya Yanga inapita kwenye kipindi cha mpito hivi sasa tangu Mwenyekiti wake, Yusuph Manji apate matatizo binafsi zaidi ya mwezi mmoja ulopita.

Imeripotiwa kuwepo kwa madai ya wachezaji ambao hawajalipwa stahiki zao za mishahara huku wemngine mikataba yao ikiwa ukingoni na huku kukiwa hakuna jitihada zozote zilizofanyika kuinusuru klabu na hali hiyo.

Baadhi ya wanachama wamezungumza na saluti5 na wameonyesha masikitiko kwa matajiri hao kuwa kimya hadi kipindi hiki ambacho walitakiwa kuonyesha mapenzi yao kwa klabu baada ya Mwenyekiti kupata matatizo.

“Yanga ina matajiri wengi hilo halina kificho lakini inasikitisha kuona wamekaa kimya hawataki kusaidia timu na wanajua wazi kuwa Mwenyekiti amepata matatizo binafsi,” alisema Ally Juma wa Mbagala mwanachama wa klabu hiyo.

“Hiki ndio kipindi ambacho matajiri hao walistahili kuinuka na kuibeba  Yanga ili kuonyesha kwamba haina utegemezi wa mtu mmoja, lakini ajabu nao wamekaa kimya na timu wameachiwa viongozi.”


Klabu ya Yanga inaongoza kwa kulipa wachezaji wake mishahara mikubwa hali ambayo imekuwa mzigo kwa uongozi uliopo madarakani kumudu gharama za kuendeshea timu.

No comments