MANCHESTER City wako mbioni kumsaini kinda wa Barcelona, Marc Cucurella ambaye bado hajapewa mkataba na mabingwa hao wa Hispania.

Beki huyo wa kushoto mwenye umri wa miaka 18 bado hajasaini mkataba mpya na mabingwa hao watetezi wa La Liga huku dili lake la  sasa likimalizika mwishoni mwa msimu huu.

City inataka kuweka damu mpya kwenye ukuta wake wakati mabeki wake wanne wa pembeni Aleksandar Kolarov, Pablo Zabaleta, Bacary Sagna na Gael Clichy wakiwa na umri wa miaka 31 na kuendelea.

Aidha, kati ya mabeki hao wanne, watatu wako ukingoni mwa mkataba wao.USISAHAU KUBONYEZA SUBSCRIBE HAPO
LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK Saluti5

Post a Comment

 
Top
Nicolaus Trac