KING KIKI KUPEPERUSHA KITAMBAA CHEUPE PASAKA NDANI KAOLE SNAKE PARK BAGAMOYO


Mwimbaji mkongwe wa dansi King Kiki akiwa na bendi yake ya Wazee Sugu, atakuwa ndani ya Bagamoyo siku ya Pasaka.

King Kiki atatumbuiza kwenye kiota cha maraha cha Kaole Snake Park, Bagamoyo ambapo mashabiki wametakiwa kwenda na kitambaa cheupe.

“Kitambaa Cheupe” ni moja nyimbo kali za King Kiki na kila unapogigwa wimbo huo, basi mashabiki hupeperusha hewani kitambaa cheupe.

Onyesho hilo la King Kiki litakalofanyika usiku, litatanguliwa na burudani ya michezo ya watoto kwa mchana kutwa.

No comments