KING MALUU ASEMA KASALOO KYANGA, KYANGA SONGA HAWAKUWA NA MPINZANI KATIKA UIMBAJI WA MUZIKI WA DANSI BONGO

MKONGWE wa muziki katika upulizaji Saxophone “Domo la Bata”, King Maluu amewasifu waimbaji mapacha Kasaloo Kyanga na Kyanga Songa akisema hawakuwa na mpinzani katika muziki.

“Wale walikuwa ni wanamuziki hasa na ile ilikuwa fani yao, kwa sababu kwenye muziki kuna watu wanalazimisha kuimba wakati fani inaonyesha kuwakataa kabisa, lakini hilo halikuwa kwao,” alisema Maluu.


Alisema kuwa, kwa waimbaji wa dansi ambao bado wanaendelea kuutumikia muziki hadi sasa, mfano wa Kasaloo na Kyanga Songa ni Hassan Rehani wa Mlimani Park Sikinde Bitchuka na Shaaban Dede wa Msondo Ngoma Music Band ambao amedai wanazeeka mwili lakini si sauti.

No comments