KIPA WA AFRICAN LYON ANUKIA YANGA... atishia uwepo wa Barthez kikosini

YANGA ipo kwenye hatua nzuri ya kumnasa kipa hatari wa Africon Lyon, Youthe Rostand ambaye anatakiwa katika kikosi hicho kuja kuwapa changamoto wenzake wawili.

Taarifa kutoka ndani Yanga zinasema kwamba watoto hao wa Jangwani wapo katika hatua za mwisho wakijadili na mmoja wa makipa wao wa sasa ambapo uchunguzi unaonyesha huenda mkongwe Ally Mustaph “Barthez” akaachwa mwishoni mwa msimu.

Rostand amekubali kujiunga na Yanga na amesema kwamba endapo atatua katika kikosi hicho haoni kama kuna kipa atakayemnyima nafasi ya kulinda lango la timu hiyo.

Endapo Yanga inamnasa Rostand ni wazi itakuwa na makipa watatu na kuifanya nafasi hiyo kuwa na makipa watatu wenye uwezo mkubwa.


“Yanga ni timu kubwa na mkataba wangu unamalizika baada ya siku 30, ni furaha kwangu kuona nahitajika katika timu kubwa hapa lakini tusubiri kuona hili tutamaliza vipi,” alisema Rostand.

No comments