KIUNGO WA MBEYA CITY ANUKIA KIKOSINI YANGA MSIMU UJAO

KIUNGO wa timu ya Mbeya City, Kenny Aly anatarajia kuvaa jezi za Yanga msimu ujao badaa ya mkataba wake wa sasa kufikia tamati mwishoni mwa msimu huu.

Kenny alisema kwamba anaipa nafasi ya kwanza timu yake lakini ikiwa patatokea klabu nyingine yenye maslahi mapana zaidi hatasita kwasababu mpira ndio kazi yake.

“Mkataba wangu wa Mbeya City unaisha mwishoni mwa msimu huu lakini kama kutatokea timu nyingine yoyote yenye maslahi mazuri zaidi sitasita kusaini,” alisema nyota huyo.

“Mpira ndiyo kazi yangu ambayo inanifanya niweze kuendesha maisha yangu hivyo endapo itatokea timu yenye maslahi mazuri nitajiunga nayo,” alisema kiungo huyo.


Nae baba mzazi wa mchezaji huyo, mzee Ally Mwambugu alisema kuwa hana wasiwasi na kijana wake endapo ataenda kujiunga na Yanga kwasababu anaamini ana uwezo wa kucheza kwenye kikosi cha timu yoyote hapa nchini kwani mpira upo ndani ya damu yake akifuata nyayo zake.

No comments