KOCHA JOSEPH OMOG AWATULIZA PRESHA MASHABIKI WA SIMBA... awaambia "tulieni, ubingwa ni wetu"

KOCHA wa Simba, Joseph Omog amesema hana wasiwasi hata kdogo kwamba ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu utatua Msimbazi.

Omog ambaye ni raia wa Cameroon, amesema mipango yake haijaharibika kabisa baada ya kuambulia pointi saba badala ya tisa ambazo walikuwa wanazitegemea kuzivuna kwenye mechi zao za Kanda ya Ziwa katika mechi dhidi ya Kagera Sugar, Mbao FC na Toto African.

Amesema kwamba mipango ya Simba kwa sasa imeelekezwa kwenye mechi tatu za mwisho ambazo zote zitapigwa kwenye uwanja wa Taifa dhidi ya Mwadui, African Lyon na Stand United.

Omog amesema kwamba ingawa lengo la Simba ilikuwa ni kuondoka na pointi zake tisa katika Kanda hiyo, lakini walau kwa kuambulia hizo saba si jambo baya kutokana na ugumu wa Ligi katika dakika hizi za mwisho.

Simba ilianza kwa kufungwa na Kagera Sugar kwa mabao 2-1, ikaifunga Mbao FC mabao 3-2 kisha wakatoka suluhu ya 0-0 na Toto African ya Mwanza.

Hata hivyo kamati ya masaa 72 ya Shilikisho la soka Tanzania iliipa Simba ushindi wa mabao 3 na pointi 3 kwenye mechi ya Kagera Sugar kutokana na Kagera kumchezesha beki wake Mohammed Fakhi aliyekuwa na kadi tatu za manjano.

“Sio vibaya kwamba tumepata pointi saba badala ya tisa kama tulivyopanga awali, nasema hivyo kwa sababu ni bora tumeambulia pointi hizo kuliko tungefungwa kabisa kwani ingetutoa kwenye mbio za kugombania ubingwa,” amesema kocha huyo.

Amesema kwamba kwa sasa na vigumu kupata pointi kama hizo kwa sababu timu nyingi zinajinasua katika janga la kushuka daraja.


“Tulichokibakisha kwa sasa ni kupata matokeo mazuri kwenye mechi hizi zilizobaki ambazo tutakuwa na faida ya kucheza katika uwanja wa nyumbani na nina uhakika kwamba hatutakuwa na cha kupoteza kwa sababu lengo ni kupata pointi zote katika mchezo hiyo,” alisema Omog.

No comments