KOCHA LWANDAMINA AAPA KUIPIGANIA YANGA MICHUANO YA KIMATAIFA MSIMU UJAO

KOCHA wa timu ya Yanga, Geogre Lwandamina raia wa Zambia amesema kuwa watafanya kila linalowezekana kuhakikisha wanarejea tena kwenye michuano ya kimataifa msimu ujao.

Yanga inakamata nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara ikiwa nyuma ya Simba ambayo ipo mbele kwa michezo miwili.

“Ni kweli tumeshatolewa, hivi sasa tupo kwenye kuona tunarejeaje kwenye michuano ya CAF msimu ujao, kila mmoja anajua ugumu wa kucheza na timu za Waarabu wanapokuwa nyumbani lakini tumejifunza mengi tutaona kile ambacho kufanya sasa,” alisema Lwandamina.

"Hatujakata tamaa, nafasi ya kwenda CAF bado ipo wazi na tutahakikisha tunafanya vyema kwenye Kombe la FA na la Ligi Kuu Bara ili kurejea kwa kishindo kwa mara nyingine,” aliongeza kocha huyo.

“Siwezi kujisikia raha nikikosa kushiriki michuano ya Kimataifa mwakani hivyo tutafanya kila namna ili kupata nafasi hiyo."


Yanga inakabiliwa na mchezo wa FA leo Jumamosi dhidi ya Prisons ambapo inatakiwa ishinde ili ijiweke kwenye mazingira mazuri ya kutwaa ubingwa.

No comments