KOCHA LWANDAMINA APASUKA... asema migomo ya wachezaji Yanga imechangia kupoteza mechi yao dhidi ya MC Alger

KOCHA wa Yanga, George Lwandamina amesema kupoteza kwa mchezo wa juzi dhidi ya MC Alger kumechangiwa na mambo mengi ikiwemo migomo na waamuzi kuwabeba wenyeji.

Akizungumza na saluti5 akiwa Algeria, Lwandamina alisema mwamuzi wa mchezo huo hakuwa katika ubora kwa kutoamua mchezo huo kwa haki ambapo alichangia kwa kiasi kikubwa kuwatoa mchezoni wachezaji wake.

Lwandamina alisema mwamuzi huyo kutoka Guinea alikuwa na maamuzi ya wazi ya kuwabeba wenyeji, hali ambayo ilichangia wachezaji wake kujivuruga na kujitoa mchezoni.

Alisema mbali na hilo pia kitendo cha wachezaji wake kugomea mchezo huo pia kimechangia kwa kiasi kikubwa Yanga kufanya vibaya ambapo pengo la beki Vicent Bossou na mshambuliaji Obrey Chilwa yalionekana.

Kocha huyo aliwataka Wanayanga kutulia na sasa kupeleka akili zao katika mechi za Ligi akitaka kufanya kazi ya ziada kuchukua ubingwa wa Ligi msimu huu.

“Tulikuwa ugenini lakini wenzetu walipata msaada mkubwa kutoka kwa waamuzi, hawakuwa waamuzi waliokuja kuchezesha kwa haki, walituumiza sana wakawatoa wachezaji mchezoni,” alisema Lwandamina.


“Ukiangalia pia hata kitendo cha wachezaji baadhi kugoma pia kimechangia ukiangalia hatukuwa vizuri katika ulinzi lakini pia hata katika safu ya ushambuliaji kuna kitu pia kilipungua.

No comments