KOCHA LWANDAMINA ASEMA MAJERUHI YANGA HAWATAZUIA UBINGWA MSIMU HUU

KUELEKEA mechi sita za wisho za Ligi ya Vodacom, kocha wa Yanga, George Lwandamina amesema ana uhakika na ubingwa licha ya kuandamwa na majeruhi wengi msimu huu.

Lwandamina amesema ametumia kuwajenga vizuri wachezaji waliyopo kwa lengo la kuhakikisha wanabadilika na kuisaidia timu hiyo iweze kutwaa ubingwa wa Ligi hiyo msimu huu.

“Ni kweli tunao wachezaji wengi muhimu majeruhi lakini hilo halina shida wapo vijana ambao nimewajenga kipindi hiki cha mapumziko, naamini watafanya vizuri na kuutetea ubingwa wetu,” amesema Lwandamina.

Amesema Yanga ina kikosi kipana isipokuwa kinachowasumbua kwa sasa ni wachezaji hao kutoaminiwa na hivyo kujitoa katika majukumu ya kupigania timu yao na kuonekana hawna msaada.

Amesema kama kocha amejitahidi kuwarudisha kwenye hali yao ya kawaida wachezaji hao na anajivunia kwakuwa na uwezo mkubwa isipokua walipoteza hali ya kujituma kutokana na kukatishwa tama na kocha aliyekuwepo kutokana na kuwekwa benchi muda mrefu.


Yanga inayokabiliwa na kibarua kigumu cha kuwakabili MC Alger kwenye mchezo wa kufuzu hatua ya makundi ya michuano ya kombe la Shirikisho Afrika inaendelea na mazoezi yake kwenye uwanja wa polisi Dar es Salaam.

No comments