KOCHA LWANDAMINA ATAKA WACHEZAJI SABA WAPYA WAZAWA WATUE YANGA SC

YANGA imebakiza mechi tano kumaliza Ligi huku ikiwa imepania kuibuka mabingwa, lakini pia mikakati ya kuunda kikosi kipya cha nguvu imeanza kwa usiri mkubwa huku ripoti ikionyesha jumla ya vifaa saba vya ndani vinahitajika.

Taarifa kutoka ndani ya Yanga zinasema vigogo wa klabu hiyo wiki iliyopita walikukutana na kocha wa timu hiyo, George Lwandamina ambaye katika mpango wake wa awali ametaka jumla ya wachezaji wapya saba wazawa wenye uwezo wa kuhimili ushindani wasajiliwe.

Bosi mmoja wa Yanga amesema Lwandamina ametaka kazi kubwa ifanyike sasa kutafuta wachezaji hao huku wakiwasilisha majina matano ya wachezaji aliowaona katika mzunguko wa pili wa Ligi, wengine akiuachia uongozi.

Pamoja na majina hayo kufanywa siri kubwa kuhofia kuhujumiwa lakini kocha huyo katika ripoti yake ametaka kutafutiwa mabeki watatu, mmoja akiwa wa kati mmoja wa kulia na mwingine wa kushoto.

Sambamba na hao, kocha huyo pia ametaka kusajiliwa viungo wawili mmoja mkabaji na mwingine mchezaji ambapo pia ametaka winga Simon Msuva kutafutiwa msaada wa mshambuliaji mmoja wa kati.

Katika ripoti hiyo pia kocha huyo amependekeza kutafutiwa kocha mmoja lakini vigogo hao wamefanya siri kubwa kuwa kocha yupi anaweza kuachwa katika kikosi hicho huku uongozi ukikubali ushauri wake.

“Kiukweli kocha ametupa ripoti yake itakavyokuwa na awali ametaka atafutiwe wachezaji saba wapya na kati ya hao anataka wengine waangaliwe kwanza wazawa lakini wakikosekana ndiyo tuangalie nje,” alisema bosi huyo.


“Tumezungumza na kocha kiukweli tumemkubali kwanza kikubwa alichotuvutia ni mvumiulivu kwa matatizo tuliyoyapitia hapa kati, angekuwa kocha wakizungu ameshatuaga lakini amevumilia kwa kiwango kikubwa."

No comments