KOCHA MWAMBUSI AWAPONDA WACHEZAJI WAKE YANGA... asema hajaridhika na kiwango walichoonyesha dhidi ya MC Alger

KOCHA msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi amesema hajaridhika na kiwango kilichoonyeshwa na wachezaji wake licha ya kuwa na goli 1-0 dhidi ya MC Alger kwenye mchezo wa Kombe la shirikisho Afrika.

Mwambusi amesema wanahitaji kupandisha kiwango chao angalau kifike asilimia 65 ili kuwa kwenye nafasi nzuri zaidi.

“Bado sijaridhika kwa sababu tunatakiwa tupandishe kiwango chetu angalau tufike asilimia 65 tunaweza kuwa katika kiwango ambacho kinatakiwa zaidi.”

“Tulikuwa na majeruhi lakini nao wameanza kurudi tunategemea watarudi zaidi, kwenye mechi ya marudiano watazidi kupona.”

Mwambusi pia akazungumzia kuhusu wachezaji wake kupoteza nafasi nyingi za kufunga na kushindwa kutumia vyema faida ya kucheza kwenye uwanja wa nyumbani.

“Tulikosa utulivu dakika ya mwisho tulipata nafasi kama Kessy angeamua kumpa Msuva tungekuwa tunatengeneza goli la pili lakini tumeshayaona hayo na kwasababu tumeshinda 1-0 mengine tutayafanyia marekebisho katika siku chache hizi kabla ya mechi ya marudio.


Wachezaji wanatakiwa kutengeneza nafasi nyingi za kufuka kwenye eneo lsa goli ili kuwa na maamuzi sahihi kama tulivyo funga goli lka kwanza ili kuwa na maamuzi magoli yafungwe kwa namna hiyo.

No comments