KOCHA WA YANGA ASEMA USHINDI WA BAO 1-0 DHIDI YA AZAM FC NI ISHARA MBAYA KWA ALGER

KOCHA wa Yanga George Wandamina amesema ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Azam ni ishara mbaya kwa MC Alger kwamba hawatatoka salama.

Akizungumza na Saluti5 Lwandamina alisema ushindi wa wazi umeongeza morali katika kikosi chake na kwamba wanataka kuhakikisha wanajipanga vyema kushinda kwa mabao zaidi ya mawili ili kujiweka vyema kabla ya mchezo wa marudiano.

Lwandamina alisema kamwe hajawahi kuziogopa timu za Uarabuni ambapo ajawahi kupoteza mechi yoyote akiwa nyumbani ambapo wanataka kutumia dimba lao la uwanja wa Taifa siku ya jumamosi ya tarehe 8 kupata matokeo mazuri yatakayowapa wepesi ugenini.

“Tumeshinda mechi muhimu dhidi ya timu ngumu Azam sasa tunataka kutumia morari hiyo kuweza kushinda dhidi ya MC Alger, tuna kila sababu ya kupata matokeo hayo,” alisema Lwandamina.


“Najua ugumu wa kuwaumiza timu za Uarabuni nimekutana nazo mara kadhaa najua tufanye nini ili tuwaondoe.

No comments