KOCHA ZIDANE APATWA NA MCHECHETO WA KUTUPIWA VIRAGO REAL MADRID

KOCHA wa timu ya Real Madrid Zinedine Zidane amekiri kuwa hana uhakika wa kibarua chake ndani ya ya klabu hiyo na ndiyo maana hadi sasa hajaanza maandalizi kuhusu michezo ya kujiandaa na msimu ujao wa Ligi.

Zidane anaongoza Ligi hadi sasa lakini amekuwa akipata presha kubwa kuitokana na ukubwa wa timu hiyo na hii imempelekea kocha huyo kusema yuko tayari kwa jambo lolote lile litakalotokea mwishoni mwa msimu.

“Siko salama hapa ninacho fanya kwa sasa ni kuhakikisha tunamaliza michezo iliyobaki salama nina jua vyema ni nini haswa kuifundisha Real Madrid na hivyo niko tayari kwa lolote litakalotokea,”alisema Zidane.

Madrid hawajawahi kubeba ubingwa wa Ligi Kuu Hispania tangu msimu wa mwaka 2012 lakini msimu huu wanaonekana kama wanaukaribia ila hiyo haitoshi kumuweka salama katika msimu ujao wa Ligi ya Hispania.

Wachambuzi wengi pamoja na wachezaji wa Real Madrid wamekuwa wakimpa ushirikiano Zidane kiungo wa ujerumani Toni Kroos amesema moja kwa moja kwamba Zidane ni mtu sahihi kwao na watafurahi kama atabaki katika klabu hiyo.


“Nafurahia sana kucheza chini yake ni mtu ambaye anatusikiliza kila wakati na anatuipa nafasi ya kupanga naye nini cha kufanya, toka amekuja hapa tunacheza vizuri na tunafurahia aina ya uchezaji wetu,” alisema Kroos.

No comments