"KOMANDOO" HAMZA KALALA AUNGANA NA RASHID PEMBE, ZAHIR ALLY NA KING MALUU KUUTETEA MUZIKI WA DANSI

MKONGWE wa muziki wa dansi, Hamza Kalala “Komandoo” ametia msisitizo kuwa muziki wao bado una nafasi yake kwenye jamii na kwamba dhana ya kuwa umepoteza msisimko inavumishwa na baadhi ya wadau wenye maslahi na mitindo mingine ya muziki Bongo.

Kalala amesema kuwa, dansi haliwezi kufa kwakuwa, kwa upande wake ndio muziki wa ukweli zaidi kati ya mitindo yote hapa nchini na kwamba vishindo vya kuibuka na kupotea kwa mitindo mingine vilikuwepo tangu zamani.


Kauli ya kwamba dansi bado liko hai na haliwezi kufa, imekuwa ikiongelewa na wasanii wengi wa dansi, ambapo kwa hivi karibuni wakongwe Rashid Pembe, King Maluu na Zahir Ally Zorro nao waliitilia mkazo.

No comments