KWA KAULI HII YA WENGER, SANCHEZ HAWEZI KUBAKI ARSENAL


Arsene Wenger amesisitiza kuwa  Arsenal haitavunja benki ili kumzuia Alexis Sanchez Emirates Stadium.

Mshambuliaji huyo wa Chile amebakiza mwaka mmoja kumaliza mkataba wake Arsenal na ubora wa kiwango chake msimu huu umevutia macho ya vilabu kama Paris St Germain, Chelsea na Manchester City.

Sanchez pia ametajwa miongoni mwa wachezji sita wanaowania tuzo ya mwanasoka bora wa mwaka England baada ya kufunga magoli 22 na kuchangia mara 17.

Pamoja na yote hayo Wenger hayupo tayari kumwaga kitita kizito ili kumshawishi nyota huyo asiondoke Arsenal.

Wenger amesema: "Kuna namna nyingi ya kufanya hapa. Baadhi ya watu wananiambia nimpe anachotaka, lakini hatuwezi kuheshimu kila utashi wa mshahara na kuitia klabu matatizoni.

"Ndio maana unatakiwa kufanya maamuzi chanya. Siku zote lazima klabu iwe kipa umbele namba moja.

"Naelewa  pia kuwa wachezaji wa kiwango cha juu pia ni kipaumbele chetu, laki mwisho wa siku hata kwa wachezaji muhimu ni lazima uwalipe kwa kile unachomudu".


No comments