Habari

LICHA YA USHINDI LAKINI MASHABIKI BADO WANATAKA WENGER AONDOKE ARSENAL

on

Arsenal imeshinda 2-1 dhidi ya Middlesbrough na kupanda hadi nafasi ya tano kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya England, lakini bado baadhi ya washabiki wa klabu hiyo wanataka kocha Arsene Wenger atimke.
Pamoja na kuzoa pointi tatu, lakini Arsenal haikucheza vizuri na mara kadhaaa walinusurika kufungwa kama si uimara wa kipa Petr Cech.
Alexis Sanchez alifunga kwa free-kick dakika ya 42 huku Alvaro Negredo  akiisawazishia Middlesbrough dakika ya 50.
Petr Cech akainyima Middlesbrough bao la pili kwa kuokoa kiufundi mpira wa kichwa uliopigwa na Daniel Ayala kabla Mesut Ozil hajaipatia Arsenal goli la ushindi dakika ya 71.
Middlesbrough: (4-3-2-1): Guzan 6.5; Barragan 7, Gibson 7, Ayala 6.5, Fabio 6 (Friend 17, 7); Clayton 6.5, De Roon 6.5 (Gestede 79), Leadbitter 7; Ramirez 6.5 (Traore 68, 6), Downing 7; Negredo 7
Arsenal: (3-4-2-1): Cech 7; Gabriel 6.5, Koscielny 6.5, Holding 6.5; Oxlade-Chamberlain 7, Xhaka 6, Ramsey 6, Monreal 6; Sanchez 7.5 (Coquelin 90), Ozil 7 (Bellerin 90); Giroud 6
Mabango yakimtaka kocha Arsene Wenger atimke

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *