LINAH ASEMA ALIFICHA JINA LA MTU ALIYEMPA UJAUZITO KWASABABU ZA TOFAUTI YA KIDINI

NYOTA wa muziki wa kizazi kipya, Linah amesema kwamba hakuwa tayari kuweka wazi jina la mtu aliyempa ujauzito baada ya kukataliwa na wazazi wake kwasababu ya tofauti ya dini.

Akizungumza na chombo kimoja cha habari hapa nchini Linah alisema kuwa ilimuwia vigumu kuweka wazi jina la mpenzi wake kwasababu nyumbani hawakutaka kwasababu ya masuala ya dini.

“Mimi mikristo na mwenzangu yupo dini nyingine hali iliyosababisha kuwekewa pingamizi na wazazi wangu,” alisema staa huyo.


Hivi sasa ni vigumu kuniingilia baada ya kuunganishwa kuwa mwili mmoja na mpenzi wangu baada ya wazazi kuridhia mahusiano yetu hivyo nawashukuru sana.”

“Nimebeba ujauzito katika muda mwafaka kwangu na mwenzangu yupo tayari. Mashabiki wategemee ndoa muda wowote.” 

No comments