LIVERPOOL MWENDO WA KINYOGA, YABANWA NA BOURNEMOUTH

Liverpool imeendelea kuwa na mwendo usiotabirika katika Premier League baada ya kulazimishwa sare ya 2-2 na Bournemouth.

Iliwachukua dakika saba Bournemouth kuwaduwaza Liverpool kwa bao la Benik Afobe lililodumu hadi dakika ya 40 pale Philippe Coutinho alipofunga na kufanya timu hizo ziende mapumziko kwa sare ya 1-1.

Divock Origi akaifungia Liverpool bao la pili dakika ya 59 lakini Joshua King akaisawazsihia timu yake dakika ya 87.


No comments