LWANDAMINA ASEMA "HAWATAPAKI BASI" MCHEZO WA MARUDIANO DHIDI YA MC ALGER

KOCHA wa timu ya Yanga, George Lwandamina raia wa Zambia amesema kuwa hawana mpango wa kucheza soka la kujihami katika mchezo wao wa marudio dhidi ya MC Alger ya nchini Algeria, ambayo ilichapwa bao 1-0 katika mchezo wa awali uliofanyika kwenye dimba la uwanja wa taifa Dar es Salaam.

Yanga ambayo ilishinda mchezo wa awali inatarajia kurudiana na Waarabu mwishoni mwa wiki hii huku kocha wa kikosi hicho akisisitiza kucheza soka la kushambulia zaidi kuliko kujihami.

“Hatutacheza soka la kujihami kama watu wanavyodhani badala yake tutafungua uwanja na kutengeneza nafasi nyingi za kufunga,” alisema Lwandamina.

“Mchezo wa awali tulijaribu kutengeneza nafasi nyingi za kufunga lakini tutatumia moja kupata bao, tatizo ambalo nimeliona na tayari nimeanza kulifanyia kazi,” aliongea kocha huyo.

“Hayakuwa matokeo mabaya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 nyumbani lakini lazima tubadilike na tutumie vyema nafasi katika mchezo wa ungenini maana haitakuwa kazi rahisi.”

Mabigwa hao watetezi wa Ligi kuu Tanzania Bara walifanikiwa kupata bao moja lililofungwa na Thaban Kamusoko baada ya kazi nzuri iliyofanywa na Mzambia Obrey Chirwa.

No comments