MADEE KUMBWAGIA FID Q MIKOBA YA URAIS WA MANZESE TAKAPOAMUA KUNG'ATUKA

STAA wa muziki wa kizazi kipya, Madee ambaye anatamba na kibao “Hela”, amesema kuwa atakapoachia urais wa Manzese atamrithisha mwana HipHop, Fid Q ambaye asili yake ni mkoa Mwanza.

“Kama itatokea siku naondoka manzese na kuachana na urais, basi nitamwachia kiti changu cha utawala Fid Q,” alisema msanii huyo.

“Ukiachiliambali masuala ya sanaa, Fid Q ni mtu mzima anayejitambua sana ukilinganisha na wasanii wengine ninaowafahamu,” aliongeza rapa huyo.

Made alidai kuwa “Ngosha” ndie msanii mwenye uwezo wa ziada katika sanaa, ni mtu anayejielewa na anaifahamu fani ya muziki kwa siku nyingi.


Madee alitamba na kibao cha “Nani Kamwaga Pombe Yangu”, hivi sasa yuko na wimbo mwingine wa “Hela” ambao unaonekana kushika chati za juu kwenye vituo vya radio na runinga.

No comments