MAJERUHI AMISSI TAMBWE ASEMA ANAAMINI BAADA YA WIKI MOJA ATAKUWA FITI NA KUREJEA UWANJANI

MSHAMBULIAJI tegemeo wa Yanga, Mrundi Amissi Tambwe anahitaji wiki moja zaidi kabla ya kurejea kikamilifu uwanjani, kufuatia kuwa nje kwa muda mrefu kutokana na maumivu ya goti.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Tambwe alisema kwamba anaamini baada ya wiki moja atakuwa fiti kabisa kuanza mazoezi kikamilifu.

Alisema kwa sasa anafanya mazoezi mepesi tu katika gym na kukimbia ufukweni ili kuimarika taratibu, lakini kuanzia wiki ijayo anaweza kufanya mazoezi kikamilifu.

“Bado sijawa fiti kisawasawa, lakini natarajia baada ya wiki moja ndio nitakua tayari kuanza mazoezi kikamilifu,” alisema.

Tambwe aliteumia katika mchezo wa hatua ya 32 bora ya kombe la shirikisho la soka Tanzania(TFF), au Azam sports Federation Cup  (ASFC) dhidi ya Ashanti United januari 21- amekuwa akijaribu mara kadhaa kurejea uwanjani, lakini anajitonesha na kurudi kwenye m,atibabu.


Alicheza mechi ya kwanza ya Raundi ya awali ya Ligi ya mabingwa dhidi ya Ngaya Clab nchini Comoro, lakini akashindwa kucheza mechi ya marudiano Dar es salaam, kabla ya kuibuka kwenye mechi ya ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Simba Februari 25 mwaka huu siku ambayo hakuwa katika ubora wake, Yanga ikifungwa 2-1.

No comments