MAKOCHA SIMBA, MBAO FC WAMKUBALI FREDRICK BLAGNON... wasema bila yeye Mnyama angekufa

KOCHA msaidizi wa Simba, Mganda Jackson Mayanja amekiri kwamba mshambuliaji wao Fredrick Blagnon ndie aliyewaokoa vinginevyo wangeumbuka, huku kocha wa Mbao, Etienne Ndayiragije akiunga mkono kauli hiyo.

Blagnon aliingia kuchukua nafasi ya Juma Liuzio na kufanikiwa kuipatia Simba magoli mawili katika ushindi wa 3-2, mechi iliyochezwa uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza.

Mayanja alisema, mechi za Kanda ya Ziwa ni ngumu ndio maana kipindi cha kwanza hawakuweza kupata goli lakini mabadiliko yao yaliwasaidia kwavile Blagnon anaiweza mipira ya juu ambayo wachezaji wa Mbao wanaicheza.

“Mbao walitubana lakini baadae tuliusoma mchezo tukabaini kwamba Blagnon anaweza kutusaidia kwani ni mrefu na mpambanaji na ni kweli alileta matokeo ambayo wengi hawakuyatarajia,” alisema Mayanja.

Upande wa Etienno raia wa Burundi, alisema bila ya Blagnon walikuwa wamepotea, Simba wanapenda kucheza mpira wa chini ndio maana sisi tulicheza nao kwa kupiga mipira ya juu na nilijua kabisa kuwa kutompanga Blagnon kipindi cha kwanza, kungeliwatesa.”

“Mwanzoni nilikuwa na mpango wa kumtumia kipa mwingine, lakini baadae nilibadilisha mawazo nilipogundua kuwa Blagnon yuko benchi, nikaona kwavile ni mrefu ngoja nimuweke anaweza akaokoa kirahisi mipira yake ikiingizwa, japokuwa haikuwa hivyo,” alisema Etienne.

Akizungumzia magoli, Blagnon alisema: “Napenda kufunga na nilipania kufunga baada ya kuona hali ni ngumu wakati nipo benchi.”


“Hivyo nilipopata nafasi ya kucheza, sikutaka kupoteza muda wala kuitumia vibaya nafasi hiyo, Mbao sio timu mbaya, ndio maana ilitusumbua kupata ushindi.”

No comments