MALINZI AWAITA WADAU KUWANIA KWA WINGI NAFASI UCHAGUZI TFF

IKIWA imebaki miezi mitatu kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa TFF, rais wa Shirikisho hilo, Jamal Malinzi amewataka wadau wa michezo kujitokeza kwa wingi kuwania nafasi mbalimbali ili kulisogeza mbele gurudumu la mchezo wa soka nchini.

Akizungumza na vyombo vya habari, Malinzi amesema kuwa ni jambo jema ikiwa uchaguzi huo utatokana na kampeni za kistaarabu zisizokuwa na lugha za matusi na kukashifiana.

“Kila mgombea anapaswa kunadi sera zake kwa njia ya amani pasipo kutumia lugha za matusi, dharau na kejeli kwa wagombea wengine,” alisema Malinzi.

“Ni vyema kila mgombea akanadi sera zake kwa wajumbe wa mkutano mkuu, uwezo pekee ndio silaha ya kukufanya uchaguliwe,” aliongeza Malinzi.


Shirikisho la soka nchini (TFF), linatarajiwa kufanya uchaguzi mkuu Agosti 12, mwaka huu.

No comments