MAMA KIJACHO CATHERINE CHUMA “CINDY” ALIPOSALIMIA JUKWAA LA TWANGA PEPETA CLUB MASAI


Mwimbaji pekee wa kike wa Mapacha Music Band ambaye kwa sasa amepumzika kwasababu ya ujauzito, Catherine Chuma, jana usiku alisalimia jukwaa la Twanga Pepeta ndani ya Meridian Hotel (Club Masai) Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Catherine ambaye pia hufahamika kama Cindy, alikaribishwa jukwaani na kiongozi wa Twanga Luizer Mbutu na kushangiliwa na mashabiki wengi.

Mwimbaji huyo ambaye ni ‘mke’ wa Khalid Chokoraa akapiga nyimbo mbili za ‘copy’ na kuwakuna vilivyo mashabiki wa Twanga.
Catherine Chuma (kushoto) akiimba sambamba na Luizer 

No comments