Habari

MAMBO MAGUMU AZAM FC, YAWAANGUKIA MASHABIKI

on

KOCHA wa
Azama FC, Aristica Cioaba amewaomba mashabiki wa timu hiyo kuwaunga mkono
katika kipindi hiki kigumu ambapo wanakabiliana na kibarua cha kusaka nafasi ya
kushiriki kwenye Kombe la CAF mwakani huku wakiwa wamepoteza tumaini la kubeba
ubingwa wa Ligi Kuu Bara.
Njia pekee
ya Azam kucheza Kombe la CAF ni kutwaa ubingwa wa Kombe la FA kwani mbio za
ubingwa wa Ligi Kuu Bara zipo mikononi mwa Simba na Yanga.
Azam
inatarajia kumenyana na Kagera Sugar, Toto African na Mbao huku ikitakiwa
kushinda mechi hizo ili walau kujihakikishia nafasi tatu za juu.
“Tuna kikosi
imara lakini ningeomba kupata sapoti kutoka kwa mashabiki kwasababu
tunakabiliwa na ratiba ngumu mwezi huu,” alisema.

Azam
imepoteza mwelekeo kwenye michuano ya Ligi Kuu huku njia pekee kwao ni kushinda
Kombe la FA ambalo litakuwa la pili kwao baada ya kubeba ubingwa wa Kombe la Mapinduzi
visiwani Zanzibar.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *