Habari

MANARA: ACHA WAMWAGE MBOGA SISI TUTABIDUA BAKULI TUKOSE WOTE

on

WADAU wa
soka hapa nchini wanalalamika sana kwamba Shirikisho la soka hapa nchini (TFF)
linaharibu mpira wa miguu kwa kuipendelea sana Yanga katika baadhi ya mambo.
Lakini pia
klabu ya Simba imelalamika kwamba TFF wamekuwa wakiibeba sana Yanga kiasi sasa wamechoshwa na mbeleko hiyo ya TFF kwa Yanga.
Jumatatu hii Mkuu wa idara ya Habari na Mawasiliano ya klabu ya Simba SC, Haji Manara amesema
hawatishwi na wapinzani wao waliosema wanamwaga mboga kuhusiana na kupewa
pointi 3 dhidi ya Kagera Sugar na sasa kama vipi wao watabutua sahani na bakuli wakose wote.
Kauli hiyo
ya Manara imekuja kufuatia kuwepo sintomfahamu juu ya pointi 3 walizopewa Simba na Kamati ya saa 72 akisema anashangazwa na watani wao wa jadi kushikia bango
suala hilo ilihali likiwa haliwahusu.
Manara
amesema huyo wakati akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu ya
Simba kuhusiana na hali inayoendelea kuhusiana na Kamati ya sheria na hadhi
za wachezaji TFF na Simba juu ya maamuzi ya Kamati ya saa 72.
“Juzi
kiongozi mmoja wa Yanga ameongea na vyombo vya habari na kuitishia TFF kuwa wameenda
TAKUKURU na kuomba wafanye uchunguzi juu ya maamuzi ya Kamati ya saa 72, baadae
TFF wanaitisha kikao cha Kamati ya sheria na hadhi za wachezaji kupitia maamuzi
yaliyotolewa na saa 72,”amesema Manara.
“Mkwara huo wa Yanga umewatisha sana TFF sasa na sie Simba tunasema kama wao wamemwaga
mboga na sie tunabutua sahani na bakuli tukose wote sababu TFF inaonekana
kuipendelea Yanga kwa kila jambo.”
“Nani
asiyejua Kamati hiyo ya sheria na wachezasji mpaka leo haijatoa maamuzi juu ya
suala la Tambwe dhidi ya Juuko mwaka wa pili unamalizika Banda kampiga ngumi Kavilla ndani ya wiki moja uamuzi umeshatolewa, hii Kamati tunashindwa
kuielewa?” amesema Manara.
“Kagera
kukata rufaa dhidi ya Simba ndani ya wiki wameshakaa kikao kupitia taarifa
nasema hivi sisi watoto wa mjini hawatuwezi kukubali TFF inawabeba upande mmoja
tu.”

“Tunawapa
mpaka kufikia Jumatatu tarehe 24 machi TFF wawe wametoa maamuzi juu ya kesi
mbalimbali zilizopo kwenye Kamati ya sheria na hadhi ya wachezaji vinginevyo
hatukubali tutabutua sahani tukose wote.”

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *