MANCHESTER CITY KUMALIZA MSIMU MIKONO MITUPU, YANG’OLEWA FA CUP NA ARSENAL …Sanchez moto chini


Manchester City imetupwa nje na Arsenal katika michuano ya FA Cup baada ya kufungwa 2-1 kwenye mchezo wa nusu fainali uliochezwa Wembley na kwenda hadi 'extra time'.

Hii ni dalili tosha kuwa Manchester City chini ya Pep Guardiola, itamaliza msimu bila taji lolote baada ya kutolewa pia kwenye Champions League, EFL Cup huku nafasi pekee finyu  iliyobakia kwao ni Premier League ambayo inapewa nafasi kubwa kwenda Chelsea au Tottenham.

City ilikuwa ya kwanza kupata goli kupitia kwa Sergio Aguero dakika ya 62 lakini Nacho Monreal akaisawazishia Arsenal dakika kumi baadae.


Matokeo hayo yalidumu hivyo hadi dakika 90 zilipomalizika na kulazimisha mchezo kwenda hatua ya dakika 30 za nyongeza na ndipo Alexis Sanchez alipoichinja City dakika ya 101.

No comments