Habari

MANCHESTER CITY YAFUKUZA MWIZI KIMYA KIMYA … Southampton apewa 3-0

on

Kipa ‘uchochoro’ Claudio Bravo amekuwa na siku njema kwa kuokoa shambulizi kadhaa zilizoelekezwa langoni kwake, Vincent Kompany akatakata mno na kufunga moja kati ya mabao matatu huku, Sergio Aguero akifanya kilichotarajiwa.
Mambo mengi yamekuwa yakienda kombo kwa kocha Pep Guardiola  msimu huu, lakini hatimaye Jumamosi akawa na moja ya siku ambayo kila kitu chake kilikwenda murua.
Manchester City imepaa hadi nafasi  ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya England baada ya kuilamba Southampton 3-0, magoli yote yakifungwa kipindi cha pili.
Vincent Kompany ambaye msimu huu amekuwa akisota benchi kwa kusumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara, akaifungia City bao la kwanza dakika ya 55, Leroy Sane akatupia la pili dakika ya 77 kabla Aguero hajahitimisha ushindi kwa kufunga bao la tatu dakika ya 80.
Southampton (4-2-3-1): Forster, Cedric, Stephens, Yoshida, Bertrand, Davis, Hojbjerg, Ward-Prowse (Long 60 (Rodriguez 82)), Tadic, Redmond, Gabbiadini (Boufal 60). 
Man City (4-2-3-1): Bravo, Jesus Navas, Kompany, Otamendi, Clichy, Toure, Fernandinho, De Bruyne, Silva (Zabaleta 81), Sane (Sterling 86), Aguero (Iheanacho 89). 

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *