MANCHESTER CITY YAIPA AHUENI MANCHESTER UNITED … Middlesbrough yawatibulia mahesabu


Manchester City imeshindwa kutanua pengo la pointi kati yake na Manchester United baada ya kulazimishwa sare ya 2-2 na Middlesbrough katika mchezo mkali wa Premier League.

City walikuwa wanaelekea kuachia pointi zote tatu lakini mshambuliaji wao wa pauni milioni 27, Jesus akafunga goli la kusawazisha dakika ya 85.

Alvaro Negredo aliifungia Middlesbrough bao la kwanza dakika ya 38 kabla City hawajasawazisha  kwa mkwaju wa penalti iliyofungwa na Aguero dakika ya 68.


Dakika ya 77 City wakajikuta wako nyuma kwa mara ya pili baada ya Calum Chambers kufunga goli la pili.

Katika mchezo wa awali Manchester United ilalazimishwa sare ya 1-1 na Swansea kwenye uwanja wa Old Trafford.

No comments