MANCHESTER CITY YAKINGA MKONO KUMSUBIRI ALEXIS SANCHEZ


Manchester City inaamini itafanikiwa kunasa saini ya mshambuliaji  Alexis Sanchez huku Arsenal ikianza kupoteza matumaini ya kumaliza kwenye top four ya Premier League.

Mwezi mmoja uliopita,  kocha wa City, Pep Guardiola alimtaja Sanchez kama aina ya mshambuliaji anayetaka kuwa nae msimu ujao.

City wanatumia mwanya wa kukwama kwa mazungumzo ya mkataba mpya kati ya Arsenal na Sanchez ambaye amebakiza mwaka mmoja tu kwenye kandarasi yake kwa washika bunduki hao wa London.

Guardiola anaamini yuko mbioni kuungana tena na nyota huyo wa Chile aliyekuwa nae Barcelona miaka ya nyuma.No comments