MANCHESTER UNITED ROHO MKONONI KWA MANCHESTER CITY, ‘YASHANGILIA’ SARE


Licha ya Manchester City kutawala mchezo kwa asilimia 69 kwa 31, lakini bado ilishindwa kuzoa pointi tatu kwa Manchester United ambayo hakuna ubishi kuwa 'imefurahia' matokeo.

Miamba hiyo ya jiji la Manchester wakatoka sare ya 0-0 katika mchezo wa Ligi Kuu huku bao la mshambuliaji Jesus la dakika ya 90 likikataliwa kwa kuwa mfungali alikuwa ameotea kabla hajadumbukiza mpira wavuni.


Manchester United waliokuwa ugenini  walicheza pungufu kuanzia dakika ya 85 baada ya Marouane Fellaini kulambwa kadi nyekundu.

Kwa kifupi United ilicheza roho mkononi kwa karibu mchezo wote na itabidi City ijilaumu yenyewe kwa kukosa maarifa ya kuupenya ukuta wa wapinzani wao licha kuweka kambi kwenye nusu yao.

Manchester City (4-2-3-1): Bravo (Caballero 79), Zabaleta, Kompany, Otamendi, Kolarov, Toure, Fernandinho, Sterling (Jesus 86), De Bruyne, Sane (Navas 80), Aguero

Manchester United (4-3-3): De Gea, Valencia, Bailly, Blind, Darmian, Herrera, Carrick, Fellaini, Mkhitaryan (Fosu-Mensah 86), Rashford (Young 90+2), Martial (Lingard 80)

No comments