MANCHESTER UNITED YAENDELEA KUDONDOSHA POINT, TOP FOUR SASA MTIHANI …Eric Bailly naye aumia


Manchester United inazidi kujiweka kwenye mazingira magumu ya kumaliza kwenye ‘top four’ ya Premier League baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 na Swansea kwenye uwanja wa Old Trafford.

Nahodha Wayne Rooney aliifungia United bao la kuongoza dakika ya 45 kwa mkwaju wa penalti iliyokuja baada ya Marcus Rashford kuchezewa rafu kwenye box.

United ikapata pigo dakika ya 61 baada ya beki wake wa kati Eric Bailly  kuumia na nafasi yake kuchukuliwa na Matteo Darmian.

Swansea ikasawazisha dakika 71 kupitia kwa Gylfi Sigurdsson aliyepiga ‘free-kick’ iliyokwenda moja kwa moja wavuni.

MANCHESTER UTD (4-2-3-1): De Gea 5.5; Young 6.5, Bailly 6.5 (Darmian 61', 6), Blind 7, Shaw 6 (Valencia 8', 6); Carrick 6, Herrera 6; Lingard 6.5, Rooney 5 (Mkhitaryan 80'), Martial 7; Rashford 5.

SWANSEA (4-3-1-2): Fabianski 6.5; Naughton 5, Fernandez 8, Mawson 6.5, Kingsley 6; Ki Sung-Yeung 5.5 (Fer 61', 6), Britton 6 (Montero 65', 6, Olsson 72', 6), Carroll 7; Sigurdsson 7; Ayew 6.5, Llorente 6.

No comments