MANCHESTER UNITED YAMKATIA TAMAA ADNAN JANUZAJ ...yapiga hesabu za kumuuza jumla

BAADA ya kumtoa kwa mkopo, sasa klabu ya Manchester United imeamua kuanza kusikiliza ofa zitakazoletwa na klabu zitakazomtaka mshambuliaji Adnan Januzaj.

Kinda huyo yupo Sunderland kwa mkopo lakini ameshindwa kung'ara chini ya David Moyes, kocha aliyemwamini sana Januzaj wakati alipokuwa akiifundisha United.

Tangu Moyes alipotimuliwa United, Januzaj hajawahi kufurahia maisha Old Trafford na amekuwa akitolewa kwa mkopo mara kadhaa.

No comments