MANCHESTER UNITED 'YAMTEMA' ROONEY SAFARI YA UBELGIJI KUIVAA ANDERLECHT


Kocha wa Manchester United Jose Mourinho amethibisha kuachwa wa nahodha Wayne Rooney katika safari ya Ubelgiji kwenye mchezo wa Europa League utakaochezwa Alhamisi usiku.

United inacheza mchezo wa kwanza wa robo fainali mjini Brussels dhidi ya Anderlecht na iliondoka Jumatano bila Wayne Rooney.

Mourinho amesema hiyo ni kwasababu Rooney bado hajisikii vizuri kufuatia maumivu ya kifundo cha mguu licha ya kushiriki mazoezi mapema Jumatano.

No comments