Habari

MANCHESTER UNITED YATOA POLE KWA WALIOFARIKI WAKATI WAKIANGALIA MCHEZO WAO DHIDI YA ANDERLECHT

on

Watu 30 nchini Nigeri wanatajwa kufariki dunia na wengine wengi kujeruhiwa baada ya kugongwa waya wenye nguvu kubwa za umeme wakati wakitazama mechi kati ya Manchester United ya Uingereza na Anderlecht ya Ubelgiji Alhamisi usiki
Mashabiki wa soka walikuwa wamekusanyika kwenye kituo cha kutazama mechi kupitia runinga katika mji wa Calabar kusini mwa nchi hiyo mkasa ulipotokea.
Manchester United walishinda 2-1 kwenye mechi hiyo ya hatua ya robofainali ligi ndogo ya klabu Ulaya, Europa League.
Polisi nchini Nigeria wamesema watu saba walifariki na wengine 11 wakajeruhiwa na wamelazwa hospitalini, lakini chombo kimoja cha habari cha Nigeria kinasema watu 30 wamefariki dunia katika tukio hilo.
Mwandishi mmoja nchini humo ameambia BBC kwamba kisa hicho kilitokea baada ya waya wa umeme kuangukia jumba.
Taarifa nyingine zinasema kulikuwa na watu 80 kwenye jumba hilo wakati wa kutokea kwa mkasa huo.
Mancheter United imepotoa salam za pole kwa maafa hayo.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *