MANJI ASUKA MIKAKATI YA UBINGWA JANGWANI, AWAITA TENA BIN KLEB, SEIF MAGARI YANGA SC

KATIKA kuhakikisha Yanga inachukua taji la ubingwa msimu wa tatu mfululizo, Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji amefanya maamuzi ya kiume kwa kupwapa majukumu maalumu Vigogo wawili hatari waliowahi kuongoza kamati ya usajili.

Taarifa kutoka ndani ya Yanga ni kwamba Manji amewapa majukumu vigogo wawili Seif Ahmed maarufu kwa jina la "Seif Magari" na Bin Kleb ambao inaelezwa tayari wameanza kupambana kuhakikisha timu hiyo inachukua taji lake.

Bosi mmoja wa kamati ya utendaji amesema kurudi kwa Seif na Bin kumeongeza nguvu katika kamati ya mashindano ya Yanga ambapo jukumu hilo la ubingwa limeanza kufanyiwa kazi kwa kiwango kikubwa katika timu hiyo.

Katika majukumu hayo, Manji amewaaambia vigogo hao kwamba kwa sasa wanatakiwa kupambana kuhakikisha Yanga haitetereki na wakati bilionea huyo akimaliza kuweka sawa mambo yake ndani ya kampuni zake atarudi kuungana nao katika mapambano.

“Unajua maamuzi hayo mwenyekiti aliyaamua muda mrefu na hawa jamaa tayari wameeanza kufanya mikakati ya maana kuhakikisha timu inafanya makubwa, ubingwa hatutaukosa  msimu huu,” alisema kigogo hiyo.


“Unajua Serf Na Bin wanapokutana hakuna kinachopungua wanajua kupambana na katika hili tunaona kabisa ubingwa utatua hapa Jangwani, uzoefu wao katika fitna ya soka ni mkubwa lakini pia wanajua kucheza na saikolojia wa wachezaji."

No comments