MAROUANE FELLAINI AFANYA UTOTO, ALMANUSURA AIGHARIMU MAN UNITED


Marouane Fellaini aliipa msukosuko Manchester United baada ya kulambwa kadi nyekundu ya kipuuzi dakika ya 85 katika mchezo wao wa Ligi Kuu ya England uliomalizika kwa sare ya 0-0 dhidi ya Manchester City.

Sekunde chache baada ya kupewa  kadi ya njano kwa kumchezea rafu  Sergio Aguero, Fellaini akamtwanga kichwa mshambuliaji huyo wa Argentina wakati wakizozana na refarii Martin Atkinson  hakuwa na kingine cha kufanya zaidi ya kumpa kadi nyekundu.

Kuanzia hapo lango la United likawa kwenye heka heka kubwa ambapo mpira ulikuwa hakauki kwenye 18 yao.

Hata pale zilipoongezwa dakika 6 za majeruhi, United bado ililiweka lango lao rehani.

Baada ya Fellaini kutolewa kocha Jose Mourinho alilazimika kufanya mabadiliko yaliyoonyesha wazi kuwa lengo lililobakia ni kusaka sare.

Mourinho akamtoa Mkhitaryan na kumwingiza beki Fosu-Mensah kabla ya kumtoa Rashford aliyempisha Ashley Young.No comments