Mashauzi Classic  Alhamisi hii ya April 6 watakuwa na onyesho maalum ndani ya ukumbi wao wa nyumbani, Mango Garden, Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Mashauzi Classic ameiambia Saluti5 kuwa onyesho hilo ni maalum kwaajili ya mkesha wa Karume Day inayofanyika kila mwaka April 7.

“Unajua sisi tunapiga Alhamisi ambapo Ijumaa watu wanalazimika kwenda makazini, lakini kwa kuwa Alhamisi hii inaandamana na Ijumaa itakayokuwa ‘Public Holiday’ (mapumziko ya kitaifa) basi tumeamua kuwapa mashabiki wetu kitu maalum,” alisema Isha Mashauzi.

Isha amesema katika onyesho hilo kutakuwa na sapraiz tamu za wasanii waalikwa sambamba na program maalum ya nyimbo classic za ya ‘kale ni dhahabu’.

USISAHAU KUBONYEZA SUBSCRIBE HAPO
LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK Saluti5

Post a Comment

 
Top
Nicolaus Trac