MAYANJA WA SIMBA SC ASEMA HANA WASIWASI NA KIKOSI CHAKE KUHUSU KUIKABILI AZAM FC

KOCHA msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja amesema hana hofu na kikosi chake kuelekea mechi ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho maarufu kama “Azama Sports Federation Cup” watakapokutana na Azam FC wikiendi hii uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Simba wataingia uwanjani wakiwa na machungu ya kupokonywa pointi tatu na magoli matatu na Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji, baada ya kutengua maamuzi ya Kamati ya masaa 72.

Mayanja amesema kikosi chake kipo fiti na kila mchezaji ana morari ya kuona Simba inacheza michuano ya kimataifa msimu ujao wa Ligi Kuu.

“Mechi itakuwa ngumu sana, lakini kurejea kwa Abdi Banda kunanipa faraja katika sehemu ya ulinzi, ila bado safu yangu ya ushambuliaji inakosa umakini katika umaliziaji,” alisema Mayanja.


Kocha huyo raia wa Uganda alisema malengo yao msimu huu ni kuchukua ubingwa wa VPL na Kombe la Shirikisho ili msimu ujao washiriki katika michuano ya kimataifa na kwamba yeye na wenzake katika benchi la ufundi wamefanyiakazi upungufu wote na sasa wanachokitazama ni kuona Azam anaondoka na anayekuja kwenye fainali nae anaondoka pia.

No comments