MBIO ZA LEICESTER CITY ZAISHIA KWA ATLETICO MADRID


Leicester City 1-1 Atletico Madrid. Ndivyo ubao ulivyosomeka baada ya mchezo wa marudiano wa robo fainali baina ya wakali wao wa England na Hispania.


Matokeo hayo yanawang'oa Leicester kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya kufuatia kipigo cha 1-0 walichokipata katika mchezo wa kwanza uliochezwa Madrid.

Saul Niguez aliifungia Atletico katika dakika ya 26 na kudumu hadi dakika ya 61 pale Jamie Vardy alipoisawazishia Leicester City.


No comments