MBWANA SAMATTA KUREJEA UWANJANI LEO KOMBE LA EUROPA

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania anayecheza soka la kulipwa nchini Ubelgiji, Mbwana Ally Samatta anatarajia kurejea uwanjani leo kwenye mchezo wa marudiano wa Kombe la Europa dhidi ya Celta Vigo dhidi ya nchini Hispania.

Samatta aliyewekwa benchi kwa dakika zote 90 kwenye mchezo dhidi ya KV Kortrijk ambapo ilifanikiwa kushinda jumla ya mabao 3-0 lakini leo anatarajia kuingia uwanjani baada ya mapumziko mafupi.

Timu ya KRC Genk inahitaji ushindi wa angalau bao 1-0 kwenda nusu fainali baada ya kufungwa mechi ya awali kwa mabao 3-2.

Nyota huyo ameshafanikisha kucheza jumla ya mechi 51 tangu ajiunge na timu hiyo mwezi Januari, mwaka jana akitokea TP Mazembe ya DRC Kongo.


Ikiwa watafanikiwa kuingia hatua ya nusu fainali, Samatta atakuwa ameweka rekodi nyingine ya kuwa mchezaji wa kwanza kutoka Tanzania kucheza hatua hiyo kwenye michuano ya Europa barani Ulaya. 

No comments