MDOMO WA HAJI MANARA WAIWEKA SIMBA SC KATIKA HALI YA HATARI

MSEMAJI wa Simba, Haji Manara ameiweka klabu yake katika nafasi ya hatari baada ya kulishambulia Shilikisho la soka Tanzania (TFF), na Kamati ya sheria na hadhi ya wachezaji, juu ya rufaa ya klabu ya Kagera Sugar.

Manara imeishambulia TFF jana katika mkutano wake na waandishi wa habari akisema taasisi hiyo imefanya makosa kupeleka shauri hili katika Kamati hiyo chini ya wakili msomi Richard Sinantwa.

Msemaji huyo alienda mbali zaidi akimshambulia rais wa TFF, Jamal Malinzi na Katibu wake, Selestine Mwesigwa akisema wanatumia ukabila huku pia akisema ni wadau wakubwa wa Yanga.


Aidha alisema Simba haina imani na Malinzi na uongozi wake akitaka serikali kumchunguza na pia akimshambulia waziri wa Mambo ya Ndani, Mwingulu Nchemba.

No comments