MDUDU WA ‘SARE ZISIZO STAHILI’ AENDELEA KUITESA MANCHESTER UNITED


Licha ya kuongoza tangu dakika ya 37 na kuutawala mchezo kwa muda wote, lakini Manchester United ikajikuta ikiambulia sare kwa Anderlecht kwenye mchezo wa Europa League.

United ilipoteza nafasi nyingi za wazi  hadi dakika ya 86 pale 'ilipoadhibiwa' kwa wenyeji kufunga bao la kusawazisha.

Henrik Mkhitaryan aliifungia United kufuatia pasi ya Marcus Rashford huku Leander Dendoncker akiifungia Anderlecht goli la kusawasisha kwa mpira wa kichwa uliomshinda kipa Sergio Romero.

Kwa muda mrefu United imekuwa ikitoa sare katika michezo mingi ambayo ilionekana dhahiri kustahili kushinda.

ANDERLECHT: Ruben 6; Appiah 6, Mbodji 8, Nuytinck 6 Obradovic 6.5; Tielemans 6, Dendoncker 7, Stanciu 6 (Hanni 65 6.5) Bruno 5.5 (Chipciu 58 6), Kiese Thelin 6 (Teodorczyk 75 6), Acheampong 6.5

MANCHESTER UNITED: Romero 6, Valencia 7, Bailly 7, Rojo 6.5, Darmian 7, Carrick (C) 8, Pogba 6.5, Mkhitaryan 6.5 (Fosu-Mensah 90), Lingard 6.5 (Martial 63 - 6), Rashford (Fellaini 75 - 6), Ibrahimovic 6.5.

No comments