MESSI ANAPOKUWA KWENYE UBORA WAKE HAKUNA WA KUIZUIA BARCELONA ...afunga mara mbili Real Sociedad ikilala 3-2 Camp Nou


"Yes we can," ndiyo walivyokuwa wakiimba mashabiki wa Barcelona wakimaanisha kwamba kwao hakuna linaloshindikana.

Licha ya kufungwa   3-0 na Juventus katikati ya wiki kwenye Ligi ya Mabingwa, mazingira yaliyokuwa ndani ya   Camp Nou yalichangia Barcelona kuvuna pointi tatu kwa Real Sociedad kwa ushindi wa 3-2.

Inasaidia kuwa na Lionel Messi. Nyota huyo wa Kiargentina alikuwa kwenye ubora wake, akifanya atakavyo na kufunga magoli mawili ya mwanzo katika dakika ya 17 na 37 kabla Samuel Umtiti hajajifunga dakika ya 42.

Wakati kila mtu akifiri timu hizo zitaenda mapumziko matokeo yakiwa 2-1, Francisco Alcacer akaipatia Barcelona goli la tatu dakika ya 44 huku Xabier Prieto akiifungia Sociedad bao la pili dakika ya 45.

Barcelona (4-1-2-1-2): Ter Stegen 6, Roberto 8.5, Pique 6, Umtiti 6.5, Alba 6.5, Busquets 7, Rakitic 6.5, Gomes 6 (Iniesta 69, 7), Messi 9, Suarez 8, Alcacer 7.5 (Denis 80)
Unused subs: Cillessen, Digne, Mathieu, Alena, Cardona

Real Sociedad (4-2-3-1): Rulli 6, Zaldua 5.5, Martinez 8, Navas 6, Yuri 6.5, Illarramendi 7, Zurutuza 7.5 (Granero 84), Prieto 8.5, Vela 8 (Canales 6, 62), Oyarzabal 7.5, Willian Jose 6 (Bautista 79)No comments