MICHO AITABIRIA SIMBA SC UBINGWA WA LIGI KUU BARA MSIMU HUU

“TIMU ya soka ya Simba ina kikosi imara na kama watacheza hivi hadi mwisho wa Ligi basi wana nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa.”

Hiyo ni kauli ya kocha wa timu ya taifa ya Uganda
"The Cranes" Milutin Srodoevic maarufu kama "Micho".

Akizungumza na waandishi wa habari hizi kwa barua Pepe (email) kocha Micho alisema, kiklosi cha Simba cha msimu huu ni imara na kipana na wana nafasi ya kufanya vizuri kama wataendelea kucheza kama hivi sasa.

"Ndiyo, Simba wameanza msimu huu vizuri sana na wana wachezaji wenye uwezo ukilinganisha na timu nyingine. Wana nafasi kubwa ya kufanya vizuri," alisema kocha huyo raia wa Serbia ambaye pia aliwahi kuifundisha timu ya Yanga.


“Licha ubingwa Pia Simba ni wazoefu wa mbinu za michuano ya kimataifa hivyo wakifanikiwa kutwaa ubingwa ninaamini watafika mbali kimataifa,” aliongeza Micho.

No comments