MLIPUKO WAIKUMBA BASI LA BORUSSIA DORTMUND …mechi yao na Monaco yasogezwa mbele


Basi la Borussia Dortmund limekumbwa na mlipuko wa kinachodhaniwa kuwa ni bomu na kupelekea mchezo wao dhidi ya Monaco kusogezwa mbele kwa saa 24.

Mlipuko huo ulitokea wakati timu hiyo ikiondoka katika hotel waliyofikia - L'Arrivee Hotel & Spa – kuelekea kwenye dimba la Signal Iduna Park  kwenda kuikabili Monaco.

Mechi hiyo sasa itachezwa Jumatano usiku huku beki beki wa Dortmund, Marc Bartra akiripotiwa kujeruhiwa na mlipuko huo na kukimbizwa hospitalini.

Shirika la habari la AFP limeripoti kuwa vioo vya madirisha ya basi hilo vimevunjika kutokana na mlipuko huo.

Maafisa wa polisi wamesema kulitokea milipuko mitatu karibu na eneo la basi hilo.

No comments